Burudani

Video: Victoria Kimani kuja na reality show yake ‘The Rise of The Queen’, tazama Trailer

Mwimbaji wa Chocolate City Music Mkenya Victoria Kimani kwa kushirikiana na Reel TV anatarajia kuja na reality TV show yake iitwayo ‘The Rise of The Queen’ ambayo itakuwa ni series yenye mkusanyiko wa matukio mbalimbali ya behind the scenes katika shughuli zake za muziki.

Victori ambaye alikuwa Tanzania mwezi uliopita kwaajili ya kujitangaza zaidi na kuutangaza muziki wake, amekuwa akifuatana na crew yake ya production ambao wamekuwa wakirekodi matukio mbalimbali wakati wa interviews zake, studio session wakati akirekodi, pamoja na shows zake kwa miezi kadhaa iliyopita, japokuwa alipokuja Tanzania hakuongozana nayo hivyo tutayakosa matukio ya Tanzania.

Usihangaike sana kubadilisha station katika king’amuzi chako kuitafuta reality show hiyo, sababu itakuwa ikipatikana kupitia channel yake ya Youtube kila wiki, na inatarajiwa kuanza kuonekana wiki ijayo April 8. Episode mpya zitakuwa zinawekwa Youtube kila Jumanne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents