BurudaniVideos

Video: Unaweza kufanya hip hop ukiwa mwajiriwa wa serikali? Stereo ametupa jibu

Watu wengi wanaamini kuwa mtu kufanya muziki wa hip hop serious ilhali akiwa mwajiriwa wa serikali ni sawa na kuchanganya mafuta na maji.

Rapper Stereo, ambaye ni msomi wa masuala ya maendeleo ya miji amejaribu kutuelezea hali hiyo ikoje. “Serikali yetu mfumo wake wa ufanyaji kazi na utumishi hairuhusu,” anasema Stereo.

“Sio ethical mtu kuwa kama mimi, mara msanii huko, siku nyingine umevaa zako macheni halafu watu waseme ‘yule sijui anafanya kazi wizara ya fedha’ hiyo hawaruhusu kabisa. Watu wanashindwa kupata mfano kwasababu hajawahi kutokea msanii ambaye amewahi kufanya kazi serikali kabisa akawa mkubwa hivyo,” ameongeza.

Hata hivyo amesema kama ikitokea akawa na kazi serikalini anaweza kuonesha mfano wa jinsi ya kuwa rapper mfanyakazi kwakuwa ataonesha tofauti kubwa ya jinsi anavyofanya muziki wake.

Msikilize zaidi hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents