Burudani

Video: Umewaona Wamasai kwenye video mpya ya kundi la One Direction?

Kuna makala iliyoandikwa mwezi huu kwenye mtandao wa inyenyerinews.org isemayo Maasai in Tanzania: world fame but empty stomachs’ inayozungumzia umaarufu wa jamii ya kabila la wamasai duniani lake lenye umaskini mkubwa.

Wamasai wameonekana kwenye kampeni nyingi kubwa duniani na sasa wameuza sura kwenye video ya kundi maarufu la muziki la Uingereza, One Direction ‘Steal My Girl’. Kwenye video hiyo iliyofanyika Vasquez Rocks Natural Area Park jijini Los Angeles Marekani, kundi la morani wa kimasai takriban wanane wanaonekana wakicheza kwa kuruka kama walivyoozoeleka.

Mmoja kati ya vijana watano wa kundi hilo naye anaonekana katika scene tofauti tofauti akiwa amevalia nguo za kimasai na akicheza kama wao. Haifahamiki kama watu hao ni wamasai kweli ama watu tu waliovaa mavazi ya kimasai na kuigiza. Vyovyote vile, hakuna shaka kuwa Wamasai ni miongoni mwa jamii chache barani Afrika zinazoendelea kudumisha mila na desturi zake.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents