Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Bongo Movie

Video: Thea afunguka kuhusu kuitwa na kupewa deal na kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya

By  | 

Baada ya msanii mkongwe wa filamu Thea kuonekana Ijumaa hii akiwa ofisi ya Kamishna wa operesheni wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya iliyopo Upanga jijini Dar es salaam, amefunguka na kueleza nini kilimpeleka ofisini hapo baada ya watu kuanza kuhisi labda kuna kitu kinaendelea.

Akiongea na Bongo5 muda mchache baada ya kutoka ofisini hapo, Thea amedai aliitwa ofisini hapo kwajili ya kupewa deal ya kuelimisha wasanii pamoja na jamii kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.

“Tuliitwa kwa sababu ya hizi harakati za kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya baada ya kuonekana wasanii wengi wameathirika na sisi ndiyo watu ambao tunashinda nao,” alisema Thea.

Aliongeza, “Kwahiyo wameona kupitia sisi tunaweza kusikilizana wenyewe kwa wenyewe na kuwaelimisha wengine kwa sababu hii vita ni ya kila mtu,”

Muigizaji huyo alisema hivi karibuni wataweka wazi ni nini kinaendelea baada ya kukamilika kwa deal hiyo.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW