Burudani

Video: Temba azungumzia pengo la YP, waahidi kumsomesha mwanae

Mheshimiwa Temba amesema pengo la marehemu Yesaya Ambikile ‘YP’ ni kubwa kwenye kundi lao la TMK Wanaume Family.

Mh Temba akiwa na mtoto wa marehemu aitwae Ambikile
Mh Temba akiwa na mtoto wa marehemu YP,aitwae Ambikile

Temba aliiambia Bongo5 jana kuwa YP alikuwa kiungo kikubwa ndani ya kundi lao.

“Yeye alikuwa ni mbunifu sana wa stejini na studio,” amesema Temba. “Ukiangalia chorus nyingi za TMK tulizokuwa tukifanya alikuwa yeye anachangia mambo mengi sana, Hata ukiangalia staili tunazocheza nyingi alikuwa anachangia yeye, kwahiyo pengo tumepata lakini sasa sisi ni wanaume na ni binadamu tutafanyaje, tunapaswa kusahau na tunapaswa kumuombea kwa mwenyezi Mungu.”

Temba alisema kazi ya mwisho ambayo YP alifanya na mradi wa pamoja nwa TMK na Tip Top.

“Wimbo wa mwisho tuliofanya ulikuwa ni wa TMK na Tip Top tumefanya na ma-producer wa tano. Tulikuwa tunategemea tuutoe, lakini bahati mbaya mwenzetu ametangulia na wimbo haujatoka. Lakini tutautoa kwaajili ya kuenzi yale mema na kile alichoimba watu wasikie na tulikuwa hatujui kama yatafikia haya, ni kazi ya mwenyezi Mungu,”

Katika hatua nyingine kupitia ukurasa wa Instagram wa Temba alidai kuwa watajitolea kumsomesha mtoto wa marehemu.

“Mungu tupe nguvu na ujasiri kwa yote tunayokuomba mimi na kiongozi wng Said Fella na wenzangu wa tmk family tumejitolea kumsomesha ambikile mtoto wa marehemu kwa miaka 7. Na pia kama kuna mtu ana chochote kwa kumsaidia mtoto anakaribishwa,” aliandika Temba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents