MichezoVideos

Video: Stars yasononesha taifa

Taifa Stars vs Moroco

Umati wa Watanzania uliofurika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi ulijikuta ukitoka vichwa chini baada ya timu ya soka ya Taifa kufungwa bao 1-0 na Morocco katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2012.

Stars iliyokuwa ikipewa matumaini ya kufanya vizuri katika mechi hiyo baada ya kuanza kwa kutoka sare ugenini dhidi ya Algeria, jana ilishindwa kuonesha makeke yake na hivyo kujiweka kwenye wakati mgumu katika kampeni za kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika.

Taifa Stars vs Moroco

Imebakiza mechi na Afrika ya Kati kumaliza mzunguko wa kwanza. Bao la wageni lilifungwa dakika tatu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji Mounir El-Hamdaoui alitikisa nyavu kwa mpira wa kichwa.

Hamdaoui alifunga bao hilo baada ya beki wa Stars, Nadir Haroub ‘Canavaro’ kuzidiwa maarifa na Taarabt Adel aliyeuwahi mpira na kumpasia mfungaji. Stars iliyokuwa ikicheza mbele ya Rais Jakaya Kikwete ilianza vizuri mechi hiyo ambapo ilicheza kwa kasi kwa dakika 15 za mwanzo kabla ya wachezaji wake kuonekana kuchoka na kuishiwa pumzi, hali iliyowafanya wapinzani kutawala.

Taifa Stars vs Moroco

Dakika ya kwanza, Stars ilifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini shuti la Idrisa Rajab lilidakwa na kipa wa Morocco, Lamyaghiri Nadio. Katika mechi nyingine za kuwania kufuzu zilizochezwa jana, Malawi ilichanua nyumbani Blantyre baada ya kuichapa Chad mabao 6-2.

Taifa Stars vs Moroco

Matokeo hayo yanaifanya Malawi ishike nafasi ya pili katika kundi K ikiwa na pointi sita nyuma ya vinara wa kundi hilo, Botswana wenye pointi kumi. Nao mahasimu Kenya na Uganda jana walitoka sare ya bila kufungana katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo Nairobi, Kenya.

Angalia video za mechi hiyo hapa chini:

{hwdvs-player}id=1189|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1190|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1191|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1192|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1193|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1194|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents