BurudaniVideos

Video: Siamini kama Trump atamaliza miaka 4 ya Urais wake – Abela (The Amazing)

Muimbaji wa kundi la The Amazing, Abela amesema hana uhakika iwapo Rais Donald Trump atamaliza miaka minne kama Rais wa Marekani.

https://www.youtube.com/watch?v=ElJUw0e2S80&t=5s

Abela ambaye amerudi Tanzania mwaka jana baada ya kuishi Marekani kwa miaka mingi, amesema rais huyo ameivuruga Marekani katika wiki chache tu baada ya kuapishwa kama rais wa 45 wa nchi hiyo.

“Uongozi wa Trump wiki tatu tangu uanze hauonishi kuwa na faida kwa watu wa rangi, hauoneshio kuwa na faida kwa watu weupe na hauoneshi kuwa na faida kwa Mmarekani yeyote,” ameaimbia Bongo5.

“Siamini kama anaweza kumaliza miaka minne katika Urais sababu baada ya wiki tatu amesababisha kero kubwa hivyo tutaona ni muda gani atadumu,” ameongeza.

Abela ameongeza kuwa Trump ni mfanyabiashara na staa wa reality show, haoneshi kuwa na hadhi ya Urais.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents