Burudani

Video: Shilole apiga magoti live kwenye TV na kuwaomba msamaha Watanzania

Baada ya muimbaji na muigizaji Shilole kurejea nchini weekend iliyopita akitokea Ubelgiji alikoenda kufanya show pamoja na kushoot video ya wimbo wake ‘Malele’, alipata nafasi ya kuzungumza na Watanzania kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV May 22.

Ili kuwadhihirishia Watanzania kuwa ameumizwa na kile kilichotokea hivi karibuni kwenye show yake ya Ubelgiji (Ingia Hapa) , Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili alipiga magoti live kwenye TV na kuwaomba msamaha Watanzania huku akiongea kwa hisia akiwa amefumba macho kama mtu anayesali.

“Naomba mnisamehe kwa kile kitu kilichotokea kwasababu mimi sio malaika mimi ni binadamu, mwenyezi Mungu awasamehe kwa wale walioni-judge vibaya mimi, lakini mkae mkijua ilikuwa ni sehemu yangu ya kazi na ilinitokea katika ajali kama ajali zingine. Mungu awabariki sana na nawapenda kwa wale wote mnaopenda kazi yangu ya muziki kwa maana ndio inanifanya nisomeshe watoto wangu nyumbani, ndio inanifanya mimi nivae vizuri na kupendeza katika stage zenu, Mungu awabariki sana sana sana…” Alisema Shilole.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents