Habari

Video: Serikali yaomba muda wa kutoa taarifa ya mauaji yanayoendelea nchini

Baada ya mauaji ya Watanzania kwa njia ya kuchinjwa kuendelea kushika kasi nchini, serikali imeomba muda wa kutoa taarifa rasmi kuhusu mauwaji hayo.
Jenister-Mhagama-620x308

Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni wakazi wanane wa kitongoji cha Kibatini, kata ya Mzizima jijini Tanga kukusanywa kwa mwenyekiti wa kitongoji na kisha kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana.

Akitoa taarifa bungeni, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, amesema tayari Serikali imeshaanza kushughulikia kwa ukaribu suala la mauaji yanayoendelea nchini na pindi taarifa sahihi zikikamilika umma utafahamishwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents