Burudani

Video: Ripota wa TV na cameraman wapigwa risasi na kuuawa live kwenye TV!

Ripota wa TV na cameraman wake wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wakiwa live kwenye TV huko Virginia nchini Marekani.

https://www.youtube.com/watch?v=9BFFIrfiC6U

Ripota wa kituo cha runinga cha WDBJ7, Alison Parker, 24, na cameraman Adam Ward, 27, waliuawa wakati wakifanya interview kwenye mji wa Moneta.

Mtu aliyewapiga risasi ni mwajiriwa wa zamani wa kituo hicho na alipost video hiyo mtandaoni akionesha jinsi alivyowapiga risasi.

Mtu huyo ambaye jina lake ni Vester Lee Flanagan aliyejulikana kikazi kwa jina la Bryce Williams alijiua kwa kujipiga risasi baada ya tukio hilo. Alikuwa kwenye gari lililokuwa limezungukwa na polisi.

Akaunti zake za Twitter na Facebook zimefungwa tayari.

Kituo hicho kimesema mwanamke aliyekuwa akihojiwa, Vicki Gardner wa ‘Smith Mountain Lake Regional Chamber of Commerce’ alinusurika lakini alipelekwa hospitali na alihitaji upasuaji.

Akaunti ya Twitter ya Flanagan inaonesha kuwa alikuwa na ugomvi na wawili hao. Inasemakana kuwa alikuwa akilalamika kuhusu ubaguzi wa rangi na manyanyaso.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents