Habari

Video: Ripota aacha kazi akiwa anaripoti ‘live’ kwenye taarifa ya habari ya TV, ‘F**k it, I quit’

Charlo Greene, ripota wa kituo cha runinga cha KTVA_TV cha huko Alaska ameamua kutumia njia fupi ya ku-resign, baada ya kutangaza kuacha kazi akiwa anaripoti ‘live’ kwenye runinga Jumapili usiku September 21.

“F— it, I quit,” ndio nena alilotumia hewani wakati anatangaza uamuzi wa kuacha kazi na kuondoka mbele ya camera.

Kwa mujibu wa the Alaska Dispatch News, Greene siku hiyo aliripoti habari kuhusu ‘Alaska Cannabis Club’, club inayojihusisha na kuwaunganisha watu wanaotumia marijuana kwa tiba, na baada ya kumaliza kuripoti habari hiyo akajitangaza kuwa yeye ndiye mmiliki wa club hiyo na kwamba anaacha kazi kwenye kituo hicho cha TV ili autumie muda wake kupigania kuhalalisha marijuana huko Alaska.

Ghafla matangazo yalirudishwa kwa mtangazaji aliyekuwa studio (anchor), ambaye alipatwa na mshituko uliomfanya ashindwe kuendelea kuongea.

Kituo cha KTVA11 kiliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Facebook.

“Dear Viewers,

We sincerely apologize for the inappropriate language used by a KTVA reporter during her live presentation on the air tonight. The employee has been terminated.

Bert Rudman
News Director – KTVA 11 News”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents