Habari

Video: Rais Magufuli akutana na wawakilishi wa Boeing, asema serikali itanunua ndege 4

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa masoko ya Afrika na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao makuu yake nchini Marekani Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya mchakato wa serikali kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.

2

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa uchukuzi Leornald Chamriho na katibu mkuu wa wizara ya mipango na fedha, Dotto James.

Baada ya mazungumzo hayo Rais amesema serikali ina mpango wa kununua ndege nne zikiwemo kubwa tatu ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi na kuwezesha watalii kuja hapa nchini

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents