Burudani

Video: Pharrell atoa video mpya ya ‘Marilyn Monroe’, na cover yenye msichana mweusi kujibu lawama alizopata alipotoa cover ya ‘GILR’

Pharrell Williams ametoa video ya single yake mpya ‘Marilyn Monroe’ jana, pamoja na video hiyo pia ameshare cover rasmi ya single hiyo ambayo inaongea kitu kuhusiana na lawama alizopokea alipotoa cover ya album yake mwanzoni mwa mwaka huu.

Pharrell new cover

Mwanzoni mwa mwaka huu hit maker wa ‘Happy’ alipata lawama za mashabiki wake baada ya kutoa cover ya album ‘G I R L’ iliyokuwa na picha ya wasichana watatu pamoja na yeye, wakimlaumu kwa kutoweka msichana wa Kiafrika katika cover hiyo.

Jana Pharrell ametoa cover ya single yake mpya ‘Marilyn Monroe’ ambayo ina picha ya msichana wa Kiafrika ikiashiria kuwa anajaribu kuwaridhisha mashabiki ambao walimkosoa mwanzo.

Pharrell-G-I-R-L-album-cover1

Hivi karibuni Pharrell alimwambia Oprah jinsi alivyojisikia vibaya kwa kukosolewa kutoweka msichana mweusi licha ya kuwa mmoja kati ya wasichana wale ana asili ya Afrika-Amerika japo baba yake ndio mweusi huku mama yake akiwa ni mzungu hivyo kusababisha awe mweupe kwa rangi.

Tazama video ya ‘Marilyn Monroe’ iliyotoka jana

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents