Burudani

Video: Oprah Winfrey amtoa machozi Pharrell Williams kwenye kipindi cha TV

Kati ya nyimbo ambazo zimehit sana kidunia kipindi hiki ni pamoja na ‘Happy’ ya mwimbaji, rapper na producer Pharrell Williams. Mafanikio ya hit single hiyo yamemtoa machozi ya furaha mwanamuziki huyo wakati wa mahojiano na mtangazaji mkongwe Oprah Winfrey katika kipindi chake cha ‘Oprah Prime’.

Kilichomtoa machozi Pharrell ni baada ya Oprah kumwonesha video ya jinsi mashabiki wa Pharrell sehemu mbalimbali duniani walivyoupokea wimbo huo kiasi cha kuusababisha kuwa wimbo mkubwa sana na uliompa mafanikio toka ulivyotoka.

Akiwa anafuta machozi alisema, “Nashukuru kufahamu kwamba watu wameniamini kwa kipindi kirefu sana, mpaka kuweza kufikia hatua hii mpaka kujisikia hivyo”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents