Habari
Video: Operesheni ya vita dhidi ya dawa za kulevya yazaa matunda, maafisa 2 wa TRA mbaroni
Kamishna wa jeshi la polisi kitengo cha kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya , Mihayo Msikhela amefunguka na kuzungumzia mafanikio ya operesheni hiyo.
Aidha kamanda huyo alidai jeshi hilo linawashikilia maafisa wawili wa TRA aliojihusisha kupitisha kemikali bashirifu (precursor chemicals ) na b ado wawili wanatafutwa.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii kamanda huyo alidai operesheni hiyo imeweza kutekelezwa ipasavyo na wakuu wa mikoa mbalimbali.