Burudani

Video: Ommy Dimpoz ‘awasurprise’ kwa zawadi kubwa wanafunzi wa shule ya msingi Minazini walioimba ‘Tupogo’

Ommy Dimpoz ameendelea kujithibitishia mwenyewe jinsi wimbo wake Tupogo unavyopendwa si tu na vijana na watu wazima, bali hata watoto wadogo wa shule za msingi.

Msanii huyo leo ameshuhudia ukubwa wa wimbo wake huo, pale kundi kubwa la watoto wa darasa la kwanza na la pili wa shule ya msingi Minazini iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam lilivyokuwa likiuimba kwa pamoja.

Baada ya kuona jinsi watoto hao wanavyoujua kwa ufasaha wimbo wake huo aliomshirikisha,J-Martins, Ommy aliwazawadiwa wanafunzi hao zaidi ya shilingi 150,000 wagawane. Akizungumzia jinsi alivyojisikia kuwasikia watoto hao wakiimba wimbo wake, Ommy amesema anajivunia kutumia muda mrefu kuandika nyimbo zake ambazo zinaingia hadi kwenye akili za watoto wadogo.

“Kipimo cha wimbo wangu kuwa mkubwa na kufanya vizuri au kuwa hit song huwa naangalia kama watoto wanaimba au vipi,” amesema Ommy.

“Nikiona mtoto anaimba nafarijika zaidi kuliko mtu mzima kwasababu mtoto ana michezo yake ya kitoto, unajiuliza redio anasikiliza saa ngapi, lakini kwenye movements zake za kitoto anasikia nyimbo matokeo yake inamkaa kichwani, anakuwa anaimba, kwahiyo hicho ndio kitu cha faraja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents