Burudani

Video: Naweza kuimba na live bendi sema sijaamua tu – Shilole

Msanii wa muziki Shilole amefunguka kwa kudai kuwa hata yeye ni mkali wa kuimba live na bendi ila hajaamua tu kufanya hivyo.

Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa katika show ya Love, Melodies & Lights iliyofanyika weekend hii katika viwanja vya Leaders, muimbaji huyo alisema mashabiki wengi wanataka muziki wa live kwa kuwa ni muziki ambao una raha yake wakati unauangalia.

“Binafsi mimi ni mpenzi wa muziki wa live, napenda sana muziki wa live kwa sababu ni muziki fulani ambao unakupatia heshima, pia mashabiki wanafurahia kile unachokidanya,” alisema Shilole. “Mimi sijaamua tu kufanya muziki wa live na bendi lakini ni muziki ambao naweza kuufanya, lakini mashabiki wake mkao wa kula huwenda nikaanza kufanya,”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Mtoto Mdogo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents