BurudaniVideos

Video: Mwanamke wa China awa shujaa baada ya kumtandika mwanaume aliyetaka kumbaka kwenye lifti

Video ya kusisimua imesambaa mtandaoni ikimuonesha mwanamke akijitetea kwa kumpa kichapo mwanaume aliyetaka kumbaka wakati walipokuwa kwenye lifti huko China.

https://www.youtube.com/watch?v=tIKvpw1dXl8

Video hiyo inaaminika kuchukuliwa kwenye kamera za CCTV usiku siku ya April 24. Kwenye mtandao wa kijamii wa China, Weibo, video hiyo imekuwa gumzo kubwa kutokana na ushujaa wa mwanamke huyo.

Katika video hiyo mwanamke huyo anaonekana akiangalia simu yake huku mwanaume akiwa amesimama kwenye kona. Jamaa anajaribu kumsogelea msichana huyo kwa kumuinamia kama vile akitaka kumnusa. Mwanamke anampisha kabla ya kuweka simu yake kwenye mkoba.

Njemba anamsogolea tena mwanamke huyo na kumwekea mkono begani kwake akitaka kumpapasa matiti. Mwanamke huyo anakuwa mbogo kwa kumtandika kofi kali njemba huyo linalomfanya apepesuke hadi kwenye kona ya lifti hiyo.

Wakati mwanaume huyo anamrudia, anatandikwa teke la kwenye sehemu za siri kabla ya kumpa kifuti cha uso kinachompeleka chini kama gunia la mkaa.

Akiwa bado chini akiugulia maumivu makali, mlango wa lifti hiyo unafunguka na mwanamke huyo anatoka nje.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents