Michezo

Video: Mtoto wa Kluivert ajitengenezea rekodi kwenye ligi kuu ya Uholanzi

By  | 

Mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Jumapili hii mtoto wa mshambuliaji wa zamani Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert, Justin Kluivert amejitengenezea rekodi katika maisha yake ya soka baada ya kufunga goli lake la kwanza akiwa na miaka 17.

Goli hilo alilofunga Kluivert lilikuwa la kwanza kwa mchezaji huyo akicheza katika kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa ya Ajax ambapo aliisaidia timu hiyo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 wakiwa ugenini dhidi ya Excelsior.

Hiyo ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa mchezaji huyo kuanza katika kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Peter Bosz akichukua nafasi ya Kasper Dolberg aliyekuwa nje ya uwanja kwa majeraha.

Tazama goli hilo hapa chini:

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments