Diamond Platnumz

Video: Mtazame Diamond akimsifia Zari wakati akifuatiliza wimbo wa Mr Blue ‘Pesa’

Nani alidhania kuwa Diamond ni shabiki wa wimbo wa Mr Blue ‘Pesa’? Apparently staa huyo ni shabiki wa ngoma hiyo iliyomrejesha vyema mfalme wa Mapozi nchini.

Katika video ambayo Mama Kijacho Zari Tlale amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond anaonekana akifurahia kufuatiliza wimbo huo na kulipachika pia jina la Zari kwenye mstari alioungeza mwenyewe.

“Niki busy napata upepo wa bahari, niko Kunduchi nimetulia na mtoto Zari,” anasikika akirap Chibu. Mtazame hapo juu.

Kama ulikuwa hujui, Diamond na Mr Blue waliwahi kuwa na beef kisa akiwa ni Wema Sepetunga! Tunadhani kwakuwa ukurasa wa Diamond na Wema umeshafutika, wawili hawa wanaweza kuwa marafiki tena au sio?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents