BurudaniDiamond Platnumz

Video ya Diamond na Davido ‘My Number 1 RMX’ yatazamwa zaidi ya mara 69,000 toka iwekwe Youtube jana (Jan 6)

Unapozungumzia wasanii wa bongo flavour kwa sasa Diamond Platnumz is untouchable, jana (January 6) aliachia rasmi video iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake mbalimbali.

Ikiwa ni siku moja toka video mpya ya Diamond Platnumz aliyomshirikisha msanii wa Nigeria Davido katika remix ya my ‘Number One’ itoke, tayari video hiyo imetazamwa mara 69,210 katika mtandao wa Youtube kupitia channel ya Diamond Platnumz.

Mwaka jana mwishoni Platnumz alifunga safari kuelekea Nigeria kwaajili ya kufanya video hii, iliyoongozwa na director mkubwa Afrika Clarence Peters wa Nigeria.

Video ya kwanza ya ‘Number One’ original iliyofanywa Afrika Kusini na kuongozwa na Ogopa wa Kenya, iliwekwa Youtube September 2, 2013 na mpaka sasa imetazamwa mara 1,544,826 Youtube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents