Burudani

Video: Mercy Zephania akielezea alivyopata dili la kuonekana kwenye video ya Salome

Mercy Zephania amefunguka jinsi alivyolipata dili la kuonekana kwenye video ya ‘Salome’ ya Diamond ambayo mpaka sasa imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 12 kwenye mtandao wa Youtube.

Japo mrembo huyo ameonekana kuwa na jina jipya kwenye tasnia ya burudani lakini tayari ameshapiga hatua kubwa japo ana umri mdogo ikiwemo kuingia kwenye top 10 ya Miss Universe 2014 pamoja na kushiriki kwenye filamu ya Kiumeni ambayo inatarajiwa kutoka mwezi ujao.

Akiongea na Bongo5, Mercy amemtaja Hamisa Mobetto kuwa ndio aliyechangia kwa asilimia kubwa kwa yeye kuweza kushiriki kwenye video hiyo ya Salome.

“Kwanza Hamisa followed me on Instagram, I was so excited like everybody, ni mkubwa kwenye modelling halafu later on she calls me. ‘I got your number from Clemence’, he is a photographer I did work with him and that was the very first shoot ambao has opened be good for me I can say. ‘I got your number from Clemence and kuna video ya Diamond would like to be a part of it, you should come for casting.'”

Mercy ameongeza kuwa video hiyo walishoot kwa takriban masaa 18 ikiwa ni kuanzia saa tatu asubuhi mpaka majira ya saa tisa usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents