BurudaniDiamond Platnumz

Video: Meneja wa Trey Songz na Big Sean Kevin Liles asema haya mapya kuhusu Diamond

CEO wa kampuni ya KWL Management inayowasimamia wasanii wakubwa wa Marekani wakiwemo Trey Songz na Big Sean, Kevin Liles, amefunguka kwenye Twitter kuhusiana na ukaribu alionao na Diamond.

kevinliles_01

Kupitia session yake ya #AskKevinLiles, mtanzania aitwaye Sammy Gratian alimuuliza: Is Tanzanian artist, Diamond Platnumz under your management or possibly working with any artist under your management? #AskKevinLiles.”

Kevin alijibu kwa kupost video akielezea kuwa yupo karibu na Diamond kama washkaji.
“Shout outs to my friend Diamond Platnumz and my whole Tanzania crew,” anasema Kevin kwenye video hiyo.

“I love the country, I have spent some time there, I met the president, I actually had dinner with Diamond here in New York, I don’t manage him but we always friendly and help each other,” aliongeza.

DIAMOND-na-Kevin
Rais Mstaafu wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa mezani na Diamond Platnumz, Dickson Mkama na Kevin Liles jijini New York

Alimalizia kwa kusema, “Hey Diamond check out your boy, holla at me right.”
Diamond hakupuuzia ujumbe huo. Alimjibu Kevin kwa kumwandikia: Hey boss, Am Coming to America next Thursday….i will make sure i see you, thanks for your Major Support my boss.”

Kevinn

Liles aliwahi kuwa Rais wa Def Jam Recordings na Makamu Mkuu wa rais wa Island Def Jam music group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004. Aliwahi pia kuwa Makamu Mkuu wa rais wa Warner Music Group.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents