Burudani

Video: Lucci aeleza jinsi wimbo na video yake na Jokate ‘Kaka Dada ilivyopokelewa

Wiki mbili zilizopita, producer Lucci Da Don na Jokate Mwegelo waliachia video ya wimbo wao Kaka Dada uliopokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa muziki nchini.

Bongo5 ilipiga story na Lucci kutaka kufahamu namna wimbo wao ulivyopokelewa na yeye kudai kuwa wapo walioilewa na wengine wakiichukulia tofauti. Amesema video hiyo mpaka sasa imeangaliwa kwa zaidi ya mara 20,000 kwenye mtandao wa Youtube.

“I think imepokelewa vizuri, ofcourse kuna wengine ambao hawajaielewa hiyo story lakini kwenye channel yetu ya Youtube utaona kabisa kuna description tumetoa,”anasema Lucci.

“Kwahiyo wengine wanaamua kuropoka tu kwamba ‘hawa watu wana promote incest (mapenzi ya ndugu), wengine sijui ndugu vipi kivipi, hii nyimbo mmefeli’ wengine wanapenda video, hawajapenda the audio ‘mnatumia autotune sana’ lakini ukinionesha msanii mmoja wa Nigeria ambaye hatumii autotune, nakupa laki moja, ni ukweli kabisa, kwahiyo it’s just sana na it’s an art.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents