Burudani

Video: Linah azungumzia video ya Ole Themba, aeleza sababu ya kuonesha utamaduni wa kizulu

Linah amesema uamuzi wa kutumia utamaduni wa kizulu kwenye video yake ya ‘Ole Themba’ (‘tumaini’ kwa Kiswahili), ni kutanua soko la muziki na pia Afrika Kusini ni kama ndugu wa Tanzania hivyo anaamini kubalishana utamaduni ni jambo jema.

Akiongea kwenye mahojiano na Bongo5, Linah amesema video ya wimbo huo imeigharimu kampuni inayomsimania, No Fake Zone, zaidi ya dola za Kimarekani 40,000. “Kwanza kabisa tunatakiwa tujue kuwa sisi na Wasouth Africa ni ndugu tena wa kushibana ukiangalia hata kihistoria,” amesema. “Cha pili unapotaka kufanya kitu fulani kupitia mtu fulani inabidi ufanye kitu chake ili akutambue haraka ndio lengo la mimi kufanya hivi,” ameongeza.

Linah amedai kuwa kwakuwa ametumia Kiswahili zaidi kwenye wimbo huo ni rahisi watu kutambua kuwa ni msanii wa Tanzania. Lengo lingine la kufanya video hiyo kwa mujibu wa Linah ni kutanua wigo wa muziki wake na kujikusanyia mashabiki wapya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents