Bongo5 ExclusivesBurudani

Video: Kala Jeremiah: Wale Wale ni ngoma ya watu

Rapper wa Mwanza, Kala Jeremiah amesema ngoma yake iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana, Wale Wale ni ‘ngoma ya watu’.

Kala ameiambia Bongo5 kuwa tangu aiachie ngoma hiyo tayari ameshafanya zaidi ya show tano na muitikio wake anapoutumbuza jukwaani ni mkubwa.

“Wale Wale toka imetoka tayari imekuwa gumzo,” amesema Kala, “Unajua ogopa sana ngoma ambayo inaimbwa na watoto wadogo hiyo ndo huwa nyimbo ya kudumu miaka mia. Mimi naamini kabisa Wale Wale ni ngoma ya watu. Mpaka sasa hivi ina manufaa makubwa sana. Toka niitoe nimeshafanya show nne ama tano kubwa za watu wengi ambazo nimekuwa nikiona kabisa inavyopokelewa, inapokelewa kama wimbo ambao watu wanaufahamu, watu walihitaji kuuona, watu walihitaji kuujua. Kwahiyo hicho kinanipa moyo kwamba wimbo huo una nguvu ya kufanya vizuri huu mwaka ulioanza, 2014.

Kala ameongeza kuwa hafikirii kutoa wimbo mpya mapema kwakuwa bado Wale Wale inafanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents