Michezo

Video: Jose Mourinho amchana Arsène Wenger, amuita ‘bingwa wa kufeli’

Arsene Wenger ni ‘Bingwa wa kufeli’ kwa mujibu wa Jose Mourinho.

http://www.youtube.com/watch?v=lm6Bd2S42es

Meneja huyo wa Chelsea alikuwa akijibu madai ya meneja huyo wa Arsenal kuwa makocha wengine wa vilabu vya Premier League wanaonesha kupuuzia nafasi za kushinda kikombe sababu ya ‘uoga wa kufeli’. Chelsea ina pointi moja zaidi Gunners kileleni mwa ligi.

“Ni bingwa wa kufeli, si mimi,” alisema Mourinho kumuelezea Wenger ambaye timu yake haijawahi kushinda kikombe tangu mwaka 2005. “Hivyo kama kweli yupo sahihi na ninaogopa kufeli, ni kwasababu huwa sifeli mara nyingi.”

“Hivyo huenda yupo sahihi. Sijazoea kushindwa. Lakini ukweli ni kwamba yeye ni bingwa sababu miaka 8 bila kipande cha ‘silverware’, huko ni kufeli. Kama ningefanya hivyo nikiwa Chelsea ningeondoka na nisirudi tena.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents