Habari

Video: ITV News (Uingereza) yapepeleza jinsi biashara ya pembe za ndovu inavyofanyika Tanzania, yawarekodi wauzaji bila wao kujua

Timu ya kituo cha runinga cha Uingereza cha ITV News imefanya upepelezi katika soko la uuzaji wa pembe za ndovu nchini Tanzania kuonesha jinsi ilivyo rahisi kunununua bidhaa hiyo haramu.

http://www.youtube.com/watch?v=MSZ8V3Sc5Hg

Akijifanya kama mfanyabiashara kutoka China, mwandishi wa kituo hicho alizungumza na wafanyabiashara wa pembe hizo na kumhakikishia kuwa anaweza kupata oda yake pembe za ndovu sita ndani ya wiki mbili baada ya wao kuingia msituni na kwenda kuua tembo.
The team is offered more products on condition they remain “discreet”

Our team enters a market stall and asks about buying ivory
Timu ya ITV News ikiwa kwenye kibanda chenye wafanyabiashara wa pembe za ndovu ambao kwa nje wanaonekana wakifanya biashara ya vinyago na bidhaa zingine za mikono

Kamera zilizokuwa zimefichwa ziliwarekodi wauzaji hao wakiahidi kuisaidia timu hiyo kusafirisha pembe hizo kwenda nchini China.

The sellers offer to go back to the bush to secure six more tusks within two weeks
Muuzaji wa pembe za ndovu akimwambia mwandishi huyo kuwa anaweza kwenda kuongeza pembe za ndovu sita ndani ya wiki mbili kutegemea na uwepo wa fedha

Katika video hiyo, mfanyabiashara anasema kila kilo moja ya pembe ya ndovu inauzwa $700 ambazo ni takriban shilingi 112,700 za Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents