BurudaniVideos

Video: Hutaamini nyimbo za mastaa alizoandika Victoria Kimani, zipo walizoshirikishwa Timbaland na Chris Brown

Usimchukulie poa Victoria Kimani. Mrembo huyo wa Kenya aliyesainiwa na label ya Chocolate City amewahi kuwaandikia wasanii mbalimbali wa Marekani na leo kupitia Instagram amezitaja nyimbo mbili alizoziandika.

Ya kwanza ni ya wasanii wa Urusi, Timati & La La Land waliomshirikisha Timbaland. Wimbo unaitwa ‘All About The Money. Katika wimbo huo, sauti ya msichana anayesikika ni ya Victoria Kimani lakini anaonekana mwanamke wa kizungu akifuatiliza maneno (lip-sych).
“Well… it was me, until I saw the video, and this lady was lip syncing to my vocals!! #SongwriterProblems #ShytGetsReal #BlackgirlProblems #IStillLoveMe #Russia #Timati #Timbaland,” ameandika Vicky kwenye Instagram.

Wimbo mwingine ni wa msanii wa Japan, A.L aliyewashirikisha Chris Brown na Diggy Simmons.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents