Burudani

Video: Hussein Machozi arudi shule, anasomea Kenya

Hussen Machozi ameamua kuitafuta elimu atakayoitumia kama Plan B pale muziki utakapoacha kumlipa.

Akizungumza na kituo cha runinga cha Kenya, KTN kwenye kipindi cha Mdahalo Wikiendi, hivi karibuni, Hussein amesema kuna kipindi kitafika watu hawatauelewa muziki wake na hivyo atafanya kile alichokisomea.

“Kuna vitu ambavyo binadamu unatakiwa tuangalie plan B, siwezi kuimba maisha yote,yaani maisha yote kuwa naimba. Kwahiyo kuna kipindi kitafika kwamba muziki wangu watu watakuwa hawauelewi, kuna kizazi kitazaliwa na muziki mwingine kabisa. Sasa hivi nimejichimbia vizuri kwenye masomo, naendelea kiasi kwamba ikifika time ya mimi kuacha muziki kutakuwa na kitu kingine cha kufanya,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents