Habari

Video: Hakuna tena nyimbo za kidunia, Size 8 (Kenya) aokoka

Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya, Linet Munyali aka Size 8 ametangaza kuachana na muziki wa dunia baada ya kuokoka. Kuanzia sasa msanii huyo atakuwa akiimba nyimbo za injili na leo ameachia video ya wimbo wake wa kwanza wa gospel, Meteke.

Size 8 ni msanii mwenye mafanikio makubwa nchini Kenya na amekuwa akitafutwa zaidi kufanya show kuliko msanii mwingine wa kike nchini humo. Ukimtoa Avril, hakuna msanii mwingine wa kike aliyeweza kushindana naye.

581379_435820403141944_1783667162_n

Amedai kuwa aliokoka kitambo na nyimbo zake zikawa zinakinzana na imani yake ambapo pamoja na kupata fedha nyingi kutokana na show na kuwa na mashabiki lukuki moyoni hakuwa na amani. Muimbaji huyo mrembo mwenye miaka 28 ni mtoto wa baba wa Kiganda na mama wa Kikenya ambao wote ni wahubiri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents