Burudani

Video: G Nako kuachia mpya mbili ndani ya siku 14, azungumzia ujio wa kolabo za kimataifa

Msanii wa muziki wa hip hop wa kundi la Weusi, G Nako amefunguka kuzungumzia ujio wake mpya akiwa na nyimbo mbili huku zote akipanga kuziachia ndani ya wiki mbili.

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo moja kati ya hizo ni ile aliyofanya na muimbaji Jux.

“Baada ya Joh Makini kuachia Waya nafuata mimi kuna project yangu mpya iliyofanya na Jux itatoka wiki hii kama mipango ikienda kama tulivyopanga, na baada ya wiki moja au mbili nitaachia wimbo mwingine,” alisema G Nako.

Aliongeza “Watu wanahitaji muziki, tuna nyimbo chache, hakuna haja ya kutoachia muziki mzuri, unatakiwa kuangalia maudhui tu ya kazi yako,”.

Pia katika hatua nyingine rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kolabo zake za kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents