BurudaniVideos

Video: Emanuel Austin na Ben Pol wazungumza semina ya dance waliyoiandaa Alhamis hii Dar

Mwalimu wa dance (choreographer) mtanzania mwenye chuo maarufu nchini Ujerumani, Emanuel Austin atafanya semina maalum Alhamis hii jijini Dar es Salaam.

Kwenye semina hiyo anashirikiana na Ben Pol atakayekuwa host. Emanuel ameiambia Bongo5 kuwa ameandaa semina hiyo ili kuzungumza na vijana wanaopenda kucheza na kuwapa dondoo za kuifanya fani hiyo iwe biashara.

Emanuel amesema amegundua kuwa vijana wengi wa Tanzania wana kipaji cha kucheza lakini hawajui jinsi ya kukigeuza kuwa biashara. Ameongeza kuwa licha ya dance kuwa ajira kwa vijana, ina faida kubwa kiafya na kwamba katika shule yake mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi ni yule mwenye miaka 90 na ana afya nzuri.

“Nimeongea pia na dokta wa Ujerumani ni kweli kama mtu anacheza hawezi kuzeeka haraka sana. Kucheza kunaanza miaka mitatu mpaka mwisho so kila mtu anaweza kuja,” amesema.

Kwa upande wake Ben Pol amedai kuwa atakuwepo pale pia kuzungumza machache ya hamasa kwa watu watakaojitokeza. Semina hiyo itafanyika Unleashed Dance Studio iliyopo Mikocheni B kwa Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents