Burudani

Video: EBSS yatangaza mkakati mpya wa matumizi ya zawadi ya mshindi, hatotumia atakavyo

Mkurugenzi wa Benchmark Productions, Rita Paulsen amesema mshindi wa mwaka huu wa Bongo Star Search atasaini mkataba maalum na BSS wa namna fedha atakazoshinda zitakavyotumika kwa makusudi maalum ya kumsaidia kimuziki.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Madam Rita amesema kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa washindi wa BSS hawafiki popote licha kushinda fedha nyingi ambazo amesema wao huzitumia kwa matumizi mengine tofauti na muziki kama inavyotakiwa.

“Kutokana na changamoto za watu kusema kwamba washiriki hawatoki. Tumegundua kwamba mtu akipewa hela, hela anazopewa kwa kawaida anatakiwa azitumie pia kujijenga kimuziki. Lakini labda kutokana na maisha au nini, tumegundua kwamba wasanii hawawezi kutumia hizo hela kujijenga. Wanaweza kutumia kwa vitu vingi ambavyo ni mahitaji pia sijui nyumba, gari. So tumeamua mshindi anasaini contract na Management Company. Kwahiyo hela yake na management company, yeye mwenye anatoa hela yake, management company inaleta proposal, tunatengeneza video kadhaa, tunatengeneza promotion ya wimbo wako. Kutakuwa na mwanasheria na yeye mwenyewe anaauthorise ile hela inaenda kufanya hivyo vitu. Kwahiyo tumeona kama 20 percent ya hela atakazozipata itabidi zimtengenezee yeye future,” alisema.

hawa ndo washiriki walio ingia fainali
Washiriki watano waliongia fainali ambao ni pamoja na Elizabeth Mwakijambile,Melissa John,Maina Thadei,Amina Chibaba na Emmanuel Msuya

Fainali ya shindano hilo itafanyika Jumamosi hii, Escape 1 jijini Dar es Salaam ambapo wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Barnaba,Shaa,Snura,Makomando,Borabora Band pamoja na mshini wa mwaka jana Walter Chilambo

Barnaba nae akileza jinsi atakavyo fanya Show siku hiyo ya fainal
Barnaba akiongea na waandishi wa habari

Makomando nao wakionyesha Stail yao mpya inayo itwa Umeniroga watatambulisha sikuhiyo ya fainal ya BSS
Makomando nao wakionyesha Staili yao mpya, Umeniroga watakayoitambulisha siku fainali

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents