Burudani

Video: Diddy ahudhuria show ya Drake baada ya kumaliza bifu lao

Bosi wa lebo ya Bad Boy, Diddy amehudhuria kwenye ziara ya Summer Sixteen ya Drake iliyofanyika mjini Greensboro ikiwa ni siku chache baada ya kumaliza bifu lao.

drake-diddy

Wawili hao waliingia kwenye bifu hilo mwaka 2014 sababu ikiwa ni umiliki wa wimbo wa ‘0 to 100 / The Catch Up’ huku Diddy akiamini kuwa Drake amemuibia wimbo wake huo.

Ugomvi huo uliwapa maneno ya kuongea wasanii wawili wenye bifu na Drake akiwemo Meek Mill na Joe Budden kila mmoja akitumia nafasi hiyo kumchana kwenye wimbo wake. “Puffy almost caught a domestic when he smacked that bitch,” alirap Meek Mill kwenye wimbo wake wa ‘Wanna Know’.

Hata hivyo mwaka uliofuata Drake alionekana kulimaliza bifu hilo lakini Diddy alionekana kukaa kimya kwa muda wote bila kujibu lolote, kwa mujibu wa TMZ inadaiwa kuwa wasanii hao wamemaliza matatizo yao kwa maongezi yaliyofanyika kwa njia ya simu na hatimaye Diddy akahudhuria kwenye tamasha hilo la Drake.

https://youtu.be/AS_z62PGiRw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents