BurudaniDiamond Platnumz

Video: Diamond aelezea walichozungumza na meneja wa Trey Songz, Kevin Liles alipokutanishwa naye na Rais Kikwete Marekani

Hivi karibuni Diamond Platnumz alipata nafasi ya kukutana na mtu mkubwa katika industry ya muziki wa Marekani Kevin Liles, ambaye ni rais wa zamani wa Def Jam na kwasasa ni meneja wa muimbaji wa R&B Trey Songz na Big Sean.

Bongo5 ilitua Durban kwaajili ya Tuzo za MTV MAMA zilizofanyika Jumamosi iliyopita, ilipata nafasi ya kufanya Exclusive Interview na Diamond kabla ya tuzo hizo, pamoja na mengine Platnumz ameelezea walichozungumza alipokutanishwa na Liles na Rais Kikwete nchini Marekani.

“Ilikuwa ni namna ya kuangalia nafanya vipi katika soko la Amerika na dunia nzima” Alisema Diamond. “So nilipokutana na Mheshimiwa Rais akaniambia kitu gani unahitaji nikusaidie, nikamwambia connection, kila kitu ni connection njia ya kuweza kuingia katika soko la Amerika na dunia nzima, so akasema basi nitakukutanisha na mtu fulani ambaye naamini anaweza akakusaidia, so akamtafuta akampigia simu nikaonana naye(Kevin Liles)”.

Akizungumzia jinsi alivyo busy sasa hasa katika kujitangaza kimataifa:

“Nimekuwa nikienda speed sana kiukweli nimekuwa nikizunguka usiku na mchana kutafuta connection…wanasema wakati unapopatikana utumie vizuri hapo hapo unapopata sehemu hata kama kuna magoli mia piga hapo hapo mapumziko utapumzika baadae.”

Kuhusu collabo aliyoifanya na Mafikizolo:

“Nadhani kila mtu atakuwa na rights kwa upande lets say East Afrika nitakuwa na haki nayo mimi South Afrika wao, ikienda West ttakuwa tunagawana labda”.

Kuhusu wimbo mpya aliomshirikisha Iyanya na video yake kufanyika na director Mnigeria Mr Moe Musa, Diamond amesema video bado haijatoka japo imeanza kuchezwa Channel O.

“Video kiukweli kutoka bado tho nimeambiwa kuna Channel imeanza kupigwa (Channel O) sio mbaya lakini bado haijakuwa official released nitawaambia”. alisema Platnumz aka Chibu!

Leo Alhamisi (June 12) Diamond atatambulisha rasmi single yake mpya ‘Mdogo mdogo, ambayo hapo awali ilivuja kwa jina la ‘Kitorondo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents