Diamond Platnumz

Video: Diamond aeleza namna alivyouza mitumba, mafuta na kazi ya kiwandani alikolipwa 2,000 kwa siku

Kama si msanii tajiri zaidi Tanzania kwa sasa basi Diamond ndiye msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi kwa show. Lakini pamoja na kuwa hapo alipo sasa, maisha mazuri hakuyapata kirahisi hata kidogo.

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=87LKBuWkFeQ

Kupitia semina ya fursa iliyoendeshwa leo kwendana na Fiesta mkoani Tabora, Diamond ameeleza namna alivyopitia maisha magumu miaka michache iliyopita kabla hajawa Diamond Platnumz.

“Kuna kipindi nilishafanya kazi hadi sheli nilikuwa nauza mafuta, kuna kipindi nilikuwa nauza mitumba. Nakumbuka mwaka 2008/09 mwanzoni nilikuwa nafanya kazi Mikocheni kiwanda cha mabegi, kuna kufuli fulani zipo kwenye mabegi mimi nilikuwa nafunga. Kipindi hicho nauli hadi kurudi nyumbani inacost zaidi ya 1,000. Kazi yenyewe sikuwa nimeajiriwa, unafika pale bosi anachagua nani aingie katika kiwanda kwasababu hakuna aliyeajiriwa. Nalipwa shilingi 2,000 naingia saa 2 hadi saa 10, kula juu yangu nauli juu yangu, chakula kinazidi 1,000 nauli inazidi 1,000 nakosa hela ya kusave,”alisimulia.

Amesimulia pia jinsi ambavyo mama yake alikuwa akimkataza kufanya muziki na kumsisitiza asome zaidi lakini kwakuwa muziki alikuwa akiupenda aliendelea kuhangaika bila mafanikio hadi pale alipokutana na Papa Misifa aliyemsaidia kufanya video ya wimbo wake uliomtambulisha, Kamwambie.

Amesema fursa aliyoiona wazi kwenye muziki kipindi hicho ni wasanii wa Bongo Flava kutokuwa na dancers.

Sikiliza sauti hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents