Habari

Video ‘chafu’ ya Agnes wa Masogange inamuonesha mwanamke kama chombo cha starehe

By  | ‘Unaangalia na camera basi kidogo baby’, inasikika sauti ya mwanaume ambaye camera ya video aliyoishika mkononi, inamziba uso wake na kuchukua tukio linaloendelea mbele, ambalo ndilo lililofanya ageuke kuwa kama camera man wa video maarufu za ngono.
Camera inakamata tukio linalokuja kuwa gumzo nchini na bila shaka bado litaendelea kumuwinda msichana huyu mrembo mpaka uzee wake.
Picha ama video ikishasambaa kwenye mtandao haiwezi kupotea kamwe.
Ndivyo ilivyo kwenye video hii iliyopo kwenye mtandao wa Youtube kwa jina la ‘agnes masogange video ya ngono’. Video inayoendelea kupata views nyingi kila kukicha. Baada ya mwezi mmoja kuna uwezakano mkubwa wa kuwa imeangaliwa zaidi ya mara 100,000.
Camera hii Inaendelea kumchukua msichana huyu aitwaye Agnes Kutokana na kuonekana kwake kwenye video ya Masogange ya Belle 9, amebatizwa jina la ‘Agnes wa Masogange’, jina analolitumia pia kwenye mitandao ya Facebook na Twitter.
Kwenye video hii ya nyumbani anaonekana akiwa amevaa nguo za ndani zinazoficha kipande kidogo cha eneo muhimu katika umbo la mwanamke na hivyo kwa kawaida huvaliwa katika mazingira ya siri zaidi iwapo msichana atatoa nguo zake.
Agnes akiwa amevalia ‘bra’ na G-string hiyo anaonekana ameshika kochi lililopo kwenye sebule ya nyumba anayoishi huku akicheza mithili ya wale machangudoa wacheza uchi kwenye macasino ama club za usiku maarufu kwa jina la ‘stripers’.
Muziki unaosikika kwenye video hii ni kutoka kwa kundi la P-Square la Nigeria uitwao E no Easy! Agnes anaonekana kufurahia mchezo huu na akitii ombi la mwandani wake anayemrekodi na kuiangalia camera. Analikitisa vema umbo lake alilojaaliwa na mwenyezi Mungu na kuwaweka katika hali mbaya kihisia watazamaji wa kiume walioiona tape hii.
Zaidi ya Agnes na mpenzi wake, anaonekana msichana mwingine aliyekaa kwenye kochi moja wapo sebuleni hapo huku akipata chakula cha mchana.

Hili linaonekana kuwa ni tukio la kawaida kwa watu hawa. Baadaye Agnes anamsogelea mpenzi wake ambao wanabusiana kwa muda huku mrembo huyo akisikika akitoa miguno mikali ya kimahaba mbele ya mgeni huyo ambaye haijulikani kama ni rafiki, ndugu ama mfanyakazi wa ndani. Ni aibu.
Wanaziita ‘sex tape’. Mara nyingi zinapovuja na kusambaa katika mikono ya watu wengine wasiotakiwa kuziona, madhara yake huwa makubwa. Hata hivyo wapo waliopata umaarufu duniani kwa sex tape. Mfano mzuri ni Kim Kardashian na mwanamuziki wa R&B, Ray J wa nchini Marekani ambapo sex tape yao iliyoonesha tendo lenyewe la ngono, imewaingizia mamilioni ya dola baada ya kununuliwa na kampuni maarufu ya ngono iitwayo Vivid Entertainment. Bahati mbaya kwa Agnes video hii haitampa mamilioni yoyote zaidi ya kumpa fedheha ya maisha.
Agnes anamtupia lawama Sintah kwa kusambaza video hii. Hata hivyo Sintah amekanusha kufanya hivyo. Inasemekana camera iliyorekodi tukio hilo ilipotea katika mazingara yasiyoeleweka chumbani mwake na yeye akiwa nje ya nchi.
Ikiwa tayari mtandaoni, hitimisho gani watanzania wanalo? Kubwa ni kumdhalilisha mwanamke ambaye humu anaonekana kama chombo cha starehe. Maana yake ni kwamba Agnes alikuwa radhi kuvua nguo zake na kubaki nusu uchi ili kutimiza haja ya macho ya mpenzi wake aliyetaka kuliona umbo lake zuri katika ‘dirty dance’. Haijalishi kuwa umbo la mpenzi wake huliona kila wakutanapo kimwili bali alitaka kuliona vizuri kwenye camera!!
Huenda wazo hili halikumwingia akilini haraka Agnes lakini mpenzi wake alimlazimisha. Alitaka kutumiza ndoto (fantasy) za mpenzi wake huyo ambaye bado hajajulikana ni nani. Video hii inaonesha jinsi mwanaume alivyo na sauti kwa mwanamke ambapo amri yake humfanya mwanamke atii hata kama madhara yake ni makubwa.
Anayeonekana mhuni na mwenye tabia chafu ni Agnes. Lawama zinamkwepa mwanaume ambaye ndiye ‘producer’ wa video hii. Mwanaume aliyeshiriki kwa asilimia 100 katika kuzaliwa kwa wazo hili. Ukiwa kama mama ama baba unayesoma makala hii na una watoto wa kike, picha gani inakuijia kichwani baada ya kuona video hii?
Haya ndio maisha tunayowaandalia mabinti zetu? Kwanini mwanamke anadhalilishwa hivi? Kama mwanaume unampenda mke/mpenzi wako unaweza kuwa mzembe kiasi hiki? Kama utafanya, hakikisha unakuwa makini na mtunzaji mzuri lasivyo mpenzi wako atawindwa na fedheha kama ya Agnes kwa muda mrefu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments