BurudaniVideos

Video: C9 na Mr T Touch wazungumzia umoja wa wasanii wa Ruvuma ‘Bwela Kuni’

Mkoa wa Ruvuma kihistoria ni mkoa uliobarikiwa na unaofahamika kwa kuwa na wasanii wa nyanja mbalimbali wakiwemo wanamuziki, wacheza ngoma na waigizaji. Baadhi ya wanamuziki na wasanii wenye asili ya mkoa wa Ruvuma waliovuma na wanaoendelea kuvuma ni mwanamuziki mkongwe aliyekuwa akiimba nyimbo za dansi na sasa nyimbo za injili Cosmas Chidumule,marehemu Dr.Remmy Ongala ambaye baada ya kutoka Kongo aliishi katika mkoa wa Ruvuma kijiji cha Matimila na baadaye alikuja kuwa moja ya wanamuziki wa bendi ya Super Matimila.

Pia kwa sasa kuna wanamuziki na wasanii wengine wengi katika tasnia mbalimbami wenye asili ya mkoa wa Ruvuma na ambao wanafanya vizuri ambapo baadhi yao ni Professor Jay, Mrisho Mpoto, Godzilla, Shetta,Soprano, Captain John Komba, Jokate, Rose Ndauka, marehemu Juma Kilowoko (Sajuki), marehemu Recho Haule (wapumzike kwa amani)na maproducer wakubwa kama C9 Kanjenje, Mr.T Touch na wengine wengi.

Producer C9 Kanjenje ambaye ni producer mkubwa wa studio za C9 kwa kushirikiana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, injili, wasanii wa kuigiza wameona kuna haja ya kuanzisha mradi uitwao ‘Bwela Kuni’.

Bwela Kuni ni neno la kingoni lenye maana ya ‘Njoo hapa’. Wamesema hiyo ni kampeni maalum iliyoanzishwa na vijana wanaotokea na wenye asili ya mkoa wa Ruvuma.

Madhumuni ya kampeni hiyo ni kuamsha ari na hamasa ya wananchi wa mkoa huo na wenye asili ya mkoa huo na watanzania kwa ujumla kuweza kutangaza sifa zake, historia, tamaduni za watu wake, fursa mbalimbali zipatikanazo huko ikiwemo fursa za uwekezaji katika kilimo, utalii, biashara, elimu na uvuvi kupitia sanaa.

Vilevile kuweza kutangaza vipaji vya wasanii hao, uwezo wao na kujitambulisha kitaifa na kimataifa hatimaye kutumia vipaji vyao vya sanaa kama sehemu kubwa ya kujipatia ajira.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents