Burudani

Video: Birdman afunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kukosana na Lil Wayne

Mwanzilishi wa Cash Money Records, Birdman amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na kukosana na Lil Wayne ambaye alimshtaki na kumtaka amlipe dola milioni 51.

New Orleans rapper Lil Wayne sits with Birdman during the New Orleans Hornets NBA basketball game against the Miami Heat in New Orleans

Pia kumekuwepo na tetesi kuwa Birdman alipanga kumuua Weezy baada ya basi lake la ziara kushambuliwa kwa bunduki. Birdman alizungumza kwa mara ya kwanza na mtangazaji wa Power 105. 1, Angie Martinez mjini Miami.

“Wayne ni mwanangu milele. Hicho hakitakuja kubadilika,” alisema.

“Nadhani kinachoendelea ni biashara tu na mtazamo wangu ni, nitafanya chochote anachotaka kufanya. Lakini atabaki kuwa mwanangu. Hakuna kitakachobadilisha ukweli kuwa [Lil Wayne] ni mwanangu. Mwisho wa siku, chochote anachotaka kufanya, nipo naye. Huyo ni mwanangu. Ninampenda hadi kufa. Ana baraka zangu na nitamsupport kwa lolote atakalochagua kufanya,” alisisitiza.

Birdman anasema bado anazungumza na Wayne na kwamba vyombo vya habari vinalikuza jambo hilo. Pamoja na kuheshimu mawazo yake, Birdman hayupo tayari kuacha Wayne aondoke kwenye label hiyo.

“Siwezi kumwacha aende, lakini kama anataka kwenda ntaheshimu matakwa yake,” alisema. “Akisema anataka kwenda, siwezi kumzuia. Akiniambia ‘baba ni muda wa kwenda,’.. sijasikia kutoka kwenye mdomo wake.”

https://www.youtube.com/watch?v=EGLqvE_0-wc

Birdman amekanusha pia kumrushia pombe Wayne alipokuwa akitumbuiza kwenye klabu hivi karibuni. “Siwezi mwenyewe kumtupia kitu mtoto wangu.”

Kuhusu madai kuwa yeye na Young Thug walipanga kumuua Lil Wayne, Birdman alisema, “Hicho pengine ni kitu cha kijinga kabisa kuwahi kukisikia katika maisha yangu.”

Kuhusu kutakiwa amlipe Weezy dola milioni 51, Birdman alisema, “Sihisi kama ananidai dola milioni 50. Nilimpa mkataba wa zaidi ya dola milioni 100 na advance ya $60-70 million.”

Katika hatua nyingine Birdman alisema Nicki Minaj na Drake hawawezi kuondoka Cash Money.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents