Habari

Video: Beyonce aingia tena kwenye skendo ya kutumia ‘playback’ kwenye show ya ‘On The Run’ huko Paris

Kwa Bongo limekuwa ni jambo la kawaida kwa wasanii kutumia ‘playback’ kwenye show zao, ila kwa Beyonce ‘kufumaniwa’ akifanya show kwa kutumia ‘playback’ (lip-Syncing) ni habari kubwa ya skendo ambayo Radar Online wameiandika kama ‘the international icon caught red-handed in a “playback” scandal’.

http://youtu.be/-llu4373GBw

Ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja toka Queen Bey ashtukiwe amefanya ‘lip-syncing’ au ‘playback’ wakati akiimba wimbo wa taifa kwenye ‘presidential inauguration’ ya Rais Barack Obama, video mpya imevuja ikimuonesha Beyonce akitumbuiza kwenye show ya mwisho ya tour yake na Jay Z ‘On The Run’, iliyofanyika September 13 huko Paris na kujisahau kuwa anafanya playback.

Beyonce ambaye alikuwa anaimba ‘Partition’, aligundulika kuwa anagandamizia (playback) baada ya muda flani alipochuchuma karibu na mashabiki na kuondoa mic mdomoni wakati sauti yake ikiendelea kusikika ikiimba na baadae kurudisha mic mdomoni na kuendelea kuimba.

Tazama video hapo juu ujionee mwenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents