Bongo5 ExclusivesBurudaniMahojiano

Video: AY anajifunza urubani, aongelea jinsi anavyopenda kuona maji na kwanini michango ya harusi haina maana

Ndoto namba moja ya AY kabla ya kuwa msanii aliyefanikiwa ilikuwa ni kuja kuwa rubani wa ndege na sasa ameamua kutoendelea kuiota tu, bali kuiishi kabisa.

“Lengo la kwanza kulifunga mwaka huu ni hilo,”amesema AY kwenye mahojiano na Bongo5. “Urubani ni kitu nilichokuwa nakipenda na nakitamani kabla hata sijaanza muziki, ni kitu nilichokuwa nakipenda sana tokea zamani. So maisha unajua yanabadilika nikaanza kupenda vitu vingine, kupenda muziki lakini nikasema itafika siku, nitazichanga na ntahakikisha najisomesha.”

Akiongelea kuhusu kuutumia urubani katika maisha yake, AY amesema kuwa rubani ama kumiliki ndege binafsi vyote vinawezekana.

“Wanakuambia dream big, thing big. Fikiria kitu ambacho ni kikubwa zaidi ya uwezo wako. Kwahiyo naweza kusema kuwa kila kitu kinawezekana kwasababu hata wale wenye private jet wakati wakiwa wadogo au wakati hawawezi kuafford walikuwa wanafikiria kuwa kuna siku nao wanaweza kuwa na private jet, so vyote viwili vinawezekana,” amesisitiza AY.

Katika hatua nyingine, AY amesema anapenda kuona maji kuliko kawaida na ndio maana mara nyingi amekuwa akienda kupumzika kwenye kisiwa cha Mbudya.

“Unajua nyota yangu mimi ni kaa, nimezaliwa mwezi wa saba, napenda maji mno, yaani hapa ukiweka beseni natamani niingie. So ni moja kati ya hobby yangu kwenda kuenjoy. Lakini ni sehemu ambayo pia una relax, una meditate, ukiangalia mji kwa mbali maji inakufungua kichwa.”

ay majini

Akiongelea mipango ya kufunga ndoa na mchumba wake, AY amesema mipango ipo japo hawezi kuweka hadharani kwa sasa japokuwa hatochangisha michango kwakuwa haipendi.

“Unajua bora tuchangiane kwenye matatizo kuliko kwenye starehe za masaa manne halafu end of the day mnakuwa mmepigika,” amesema hitmaker huyo wa Party Zone. “Hiyo michango iko hapa tu, mbona Kenya watu wanafanya harusi nzuri na watu hawasumbuani? Oa kutokana na uwezo wako, ndo hicho nakimaanisha. Usitake kuoa unatamani mambo yawe makubwa wakati kipato chako ni kidogo, end of the day unakuwa umejikaba. Unakuta mtu anakununia sababu hujamchangia kwenye harusi. Lakini mimi nahisi ni vizuri akikuchangia kwenye matatizo, umekosa ada ya mtoto au wewe mwenyewe au mtu unaumwa au umefiwa, kuna matatizo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents