Habari

Video: Avril wa Kenya jana aligeuka kuwa msoma habari ‘News Anchor’ wa KTN

TV ya KTN ya Kenya jana iliamua kufanya ubunifu wa kuongeza/kuwavutia watazamaji wake kwa kumkaribisha Star wa kike mwimbaji Avril Nyambura kuwa msomaji wa habari (News Anchor) wa jana usiku (September 20) katika .

AvrilBG

Kama humfahamu Avril ni mmoja kati ya waimbaji wa kike wa Ogopa Djs wenye mafanikio nchini Kenya, ndiye aliyeimba hit songs Chokoza, Mama, Leo, Hakuna Yule na zingine. Mbali na muziki Avril pia ni muigizaji.

Nahisi jana hata watu ambao huwa hawapendi kuangalia taarifa ya habari hawakukosa kutazama KTN ili kuona star ambaye wamezoea kumsikia na mkumuona aki’chokoza’ katika nyimbo zake akisoma taarifa ya habari, ndio maana mimi nimeuita ubunifu wa ku’create attention’ iliyochanganya burudani na habari kwa wakati mmoja (Infotainment).

Picha ilianza mwenyeji wa Avril studio za KTN Betty Kyalo alipoanza kumuandaa Avril kisaikolojia ili kumfanya ajiskie huru japo kuwa hiyo si fani yake.

Betty alimpisha kiti cha kusomea habari na kisha akasimama pembeni na kuanza kuongea na Avril akimuuliza mambo tofauti kama anajiskiaje kwa hicho anachotaka kukifanya. Pia Betty alianza kumuuliza maswali tofauti na alichokuwa anataka kukifanya ili kumuandaa kisaikolojia hali hiyo katika fani ya habari inaitwa ‘to establish good rapport’.

Betty alimuuliza baadhi ya maswali kutoka kwa mashabiki likiwemo kama ameshawahi kuwa na celebrity crash. So ilikuwa ni two in one, interview na habari.

Baada ya hapo Betty alimuelekeza Avril jinsi ya kusoma habari, kamera anayotakiwa kutazama wakati anasoma na kisha Avril akashusha pumzi ndefu na kuanza kusoma.

Nilichokipenda katika usomaji wa Avril ni kuwa alipoanza kusoma alikuwa serious na baada ya mstari mmoja alikosea lakini hakupanic ali concentrate kisha akaomba radhi kwa kukosea na kuendelea kama vile ni msomaji mzoefu.

Kituo hicho kimeanzisha utaratibu wa kukaribisha ‘Guest Anchors’ wanaopendekezwa na watazamaji kwaajili ya kualikwa studio kusoma habari za KTN Friday Briefing na Avril ndiye alikuwa mgeni wa jana.

Tazama hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents