Habari

Video: Avril asimulia kwa mara ya kwanza jinsi alivyoanguka kwenye swimming pool wakati akitumbuiza Dar

Kwa mara ya kwanza muimbaji wa Kenya, Avril amelizungumzia tukio lililotokea miaka miwili iliyopita jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye Pool Party iliyofanyika kwenye hoteli ya Regency Park, Mikocheni.

Kwenye show hiyo ambayo rapper Prezzo pia alitumbuiza, Avril alijikuta akitumbukia kwenye bwawa la kuogelea lililokuwa mbele ya jukwaa. Bahati nzuri mrembo huyo anajua kuogelea.

“Nilikuwa naperform najifanya Beyonce, nimehit note na nimefunga macho siwezi kuwa nanotice kuwa check nilikuwa at the edge of the swimming pool,” Avril ameiamboa Bongo5.

“Mdogo mdogo najishtukia eeh mbona kuna maji kila mahali.”

Hata hivyo Avril hakuonekana kutetereka na kurudi tena kwenye jukwaa kuendelea japo alishangaa kwanini hakukuwa na mtu aliyeonesha nia ya kumuokoa. “And funny enough hakuna mtu aliyekuja kunichukua, nilijiokoa mwenyewe,” anasema.

Avril alikuwa Dar kwa siku tatu na ameshoot video ya wimbo mpya aliomshirikisha AY.

Kupitia Instagram ameandika:

Big big shout out to my Tanzanian family. Cannot begin to explain how much of a blessing this weekend has been. @benpol @fadhilikondo @rossiempangala your hospitality was something you don’t find with many people today. @aytanzania @sallam_sk you are big brothers any girl would be lucky to have..thank you so much for making things work out this weekend. @americannailstz Diana you are an incredible woman .. so happy to have met you .. @hanscana_ and team .. all I can say is wow!! Can’t wait to see the fruits of what we’ve accomplished this weekend. To all the radio and television producers and presenters who took the time to make a media tour possible @sammisago @bongo5 @millardayo @idrissyanelco @georgebantu (can’t put all y’all in here..instagram won’t let me)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents