Burudani

Victoria Kimani kuzindua album yake ‘Safari’ Nairobi, Lagos, J’Burg na pengine Dar

Baada ya kuachia single yake ya kwanza ya Kiswahili na ya kwanza kutoka album yake ijayo, Safari, Victoria Kimani amedai kuwa uzinduzi wa album hiyo utafanyika katika nchi takriban tatu.

14310740_303631536665538_1150886435_n

Akiongea na kipindi cha Mdundo Bando cha Lake FM ya Mwanza kinachoendeshwa na Kattieh, Kimani alisema kuwa Safari itatoka kabla ya mwaka kuisha.

Alisema uzinduzi wa album hiyo utafanyika Nairobi, Kenya, Lagos, Nigeria, Johannesburg, Afrika Kusini na pengine hata Dar es Salaam, Tanzania.

Album hiyo itatoka chini ya label yake Chocolate City yenye makao yake makuu Lagos.

Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents