Michezo

Verratti awaomba wachezaji wenzake wa PSG kuwa makini na Diego Costa

Kiungo wa timu ya PSG, Marco Verratti amewataka wachezaji wenzake kuwa makini na Diego Costa kwenye mechi yao ya leo.

1792002_heroa

Verratti ambaye kwa sasa anaonekana kuwa kiungo bora zaidi na uwezo wake kuimarika kila siku amekiri kuwa ukiwa na mchezaji kama Costa kwenye timu yako ni jambo jema daima.

Verratti amesema, “Napendelea soka la kuvutia, lakini kuwa na mtu kama Costa kwenye kikosi chako ni jambo jema daima, Anatumia mbinu za kivita kushinda mechi, lakini namjua, ni kijana mzuri anayeleta mabadiliko anapoingia dimbani.”

“Kama ningepewa fursa ya kuchagua niwe mchezaji gani katika kikosi cha Chelsea, nigependa kuwa Cesc Fabregas. Anakufanya uone nini maana ya mchezo, pumzi yake ni soka na unaweza kuona jinsi anavyocheza jinsi anavyoupenda mchezo,” aliongezea.

Verratti aliendelea kuwa timu yake ilicheza vibaya sana kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Chelsea na kupoteza magoli mengi japo walishinda mechi hiyo kwa magoli mawili kwa moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents