Burudani

Vanessa Mdee: Wimbo wangu ujao ni wa rap

Vanessa Mdee amesema hachagui muziki wa kufanya na kwamba kama mambo yakienda alivyopanga, wimbo wake ujao utakuwa wa hip hop (hatuna uhakika kama alizungumza kwa utani ama ni kweli atafanya hivyo).

Vanessa

Akiongea kwenye kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio, Jumanne hii wakati akitambulisha wimbo wake mpya ‘Siri’ alioshirikiana na Barnaba, Vanessa alidai kuwa yeye ni mpokeaji wa nyimbo nzuri bila kujali ni wa aina gani.

“Napenda kuonyesha kipaji changu na napenda kufanya vitu vingi sio kwamba nasema nahama. Mimi ni mpokeaji wa muziki mzuri. Nasikiliza reggae, rap, zouk, rhumba, taarab,” alisema Vanessa.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents