Burudani

Vanessa Mdee: Sasa hivi siwezi kuwa na mtoto…Ifahamu sababu

Muimbaji wa ‘Nobody But Me’ Vanessa Mdee a.k.a Vee Money ambaye hivi sasa ameweka wazi uhusiano wake na Jux ambaye ni boyfriend wake, ameweka wazi ni kipindi gani angependa kupata mtoto.

Vee n Jux

Vanessa (26) ambaye muziki wake umeanza kupata njia kwenye soko la kimataifa, amesema kuwa licha ya kuwa anapenda kupata mtoto lakini kwa sasa hayuko tayari kutokana na kuwa busy kupita kiasi.

“Sasa hivi sehemu ambayo nilipo katika maisha yangu niko very busy na kazi yaani, na nataka nikipata mtoto wangu au nikiwa tayari kupata mtoto niwe na uwezo wa kumlea sio kifedha tu lakini kuwepo katika maisha yake malezi ya mama yake ya karibu, akienda kulala nipo akiamka nipo kumchukua kutoka shuleni nipo, sasa hivi siwezi kufanya hivyo na siwezi kusema ndani ya miaka mitatu au minne mitano” Vee Money aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm.

Alipoulizwa kama anampenda sana Jux alijibu, “Sana, he is a great guy…he is my boyfriend”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents