Burudani

Vanessa Mdee: Jux ni rafiki yangu tu, hakuna zaidi

Vanessa Mdee aka Vee Money amekanusha tetesi zilizopo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Nitasubiri’ Jux.

vanessa

Siku za hivi karibuni, Vanessa na Jux wamekuwa karibu kiasi cha watu kuhisi kuwa ni wapenzi.

“Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu,” amesema Vanessa aliyecheka baada ya kuulizwa swali hilo.

“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile nyimbo ya Monefere. Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano Nahareel asingekuwa na Aika basi nahisi na yeye pia wangesema hivyo. Ila sio hivyo wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,” Vee ameiambia Bongo5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents