Habari

Vanessa Mdee apata shavu nchini Nigeria

Mwaka 2017 bado unaendelea kuwa wa mafanikio kwa Vanessa Mdee. Muimbaji huyo amepata dili jingine nchini Nigeria.

Hitmaker huyo wa Cash Madame amefanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wachache ambao watasikika katika mixtape ya watayarishaji wa muziki wa Nigeria ambao wanafanya kazi zao nchini Uingereza, Legendury Beatz.

Mixtape hiyo imepewa jina la ‘Legendury Beatz’. Kupitia mtandao wao wa Instagram, wathibitisha hilo kwa kuandika, “Of course the sexy @vanessamdee all the way from Tanzania, came through saucin on the #Afropop101 ????certainly certified!!! ????????????????????????✅ #LegenduryBeatz.”

Wasanii wengine watakaosikika katika mixtape hiyo ni pamoja na Mr Eazi, Simi, Niniola, Timaya na Wizkid (wote kutoka Nigeria) na R2Bees (Ghana).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents